Tuesday, February 5, 2013

‘ULEMAVU SIO UMASKINI’ Donatus Masau

0 comments


Naitwa Donatus Masau ni mwenyekiti wa CHAWATA wilaya ya Musoma vijijini, nimeoa na ninawatoto saba (7).

Kwaufupi nilizaliwa nikiwa mzima lakini katika udogo wangu nilianza kuugua homa, baada ya kupelekwa hospitali nikagundulika kua na ugonjwa wa Polio ambao ulipelekea miguu yangu yote miwili kushindwa kufanya kazi. Baada ya kupelekwa kwa waganga wa kienyeji ndo nikabahatika kupona mguu mmoja.
Katika mchakato wakuliendea swala la ndoa nilipata ushirikiano mzuri kutoka kwa wazazi na familia yangu. Baada ya kumaliza shule nilishauriwa kuoa, bahati nzuri akapatikana mchumba akaposwa, mahali yakatolewa na tukaoana mwaka 1987na nilifunga ndoa ya kikristu.
Kwakweli mtu mwenye ulemavu tukubali tusikubali inafikia hatua mpaka jamii ije kukuheshimu na kukuthamini ni pale unapokua unajijari we mwenyewe. Heshima yangu ya kwanza nimejikita sana kwenye ushauri, mwenzangu akikosea najaribu kumweleza kwamba hiki ulichokifanya sio sawa. Hali hii ilienda mpaka jamii yangu wakaona kuna haja ya kuniteua na kunipa ukatibu wa ukoo na hivyo naratibu shughuli zote za ukoo wangu.Kwa hali hiyo naona kama naenda vizuri na jamii yangu na wanakuja kuniomba ushauri wa mambo mbalimbali na tunaheshimiana kwakweli.
Kwa ujumla ndoto zangu ni kuona hakuna unyanyasaji kwa wenzangu na ikitokea nawahi haraka kutoa ushauri. Kwa mfano kama walemavu wenzangu najaribu sana kutafuta njia za kuwasaidia ili kutatua matatizo yanayo wakabili ili tuwe kwenye mtazamo mzuri wa maisha. Ulemavu sio umaskini ila ni bahatimbaya kua kunabaadhi ya viungo vinakua na hitilafu ila vichwa vinafanya kazi, tunaweza tukakaa tukabuni na kufanya maendeleo kama watu wengine.
Naiomba jamii itambue kwamba walemavu ni binaadamu kama walivo wao na wanataka heshima wathaminiwe, hivyo ione umuhimu wa kuwapeleka shuleni ili wapate elimu hii itawafanya wafikie hatua ya kua msaada katika jamii zao.
Taasisi za kiraia napenda kuzishauri kua zitambue yakwamba idadi kubwa ya walemavu wako vijijini hivyo zione umuhimu wa kufanya mahusiano mazuri na vijiji ambako walemavu wanahitaji misaada mbalimbali. Waje vijijini kuwaelimisha na kuwapatia mwanga watu wenye ulemavu kuliko kuishia mjini pekeake ambako unakuta idadi ya walemavu sio kubwa kama vijijini.
Walemavu nawashauri kujenga tabia ya kupenda sisi kwa sisi, mara nyingi sana mnapokua mnapendana ni rahisi kusaidiana kwenye mambo mbalimbali. Mlemavu lazima asiwe na tabia ya kuwabagua watu wengine, awapende na hii itapelekea watu kumsaidia. Lazima mlemavu aoneshe uwezo wa kutenda na sio kufanya majungu. Kitu kinachotualibia sana nikwamba watu wanasema sisi walemavu ni wakorofi! La! Ukorofi wetu unatokea pale ambapo itikadi yangu na yakwako zitakapo tofautiana, kwahyo mlemavu kama mlemavu shirikishwa na kubali mabadiliko.
Serikali naiomba iwajali sana walemavu, kwa mfano serikali imeweka sheria ya kuwasaidia na kuwalinda walemavu lakini  haikuweka angalizo la je wasipolindwa nini kifanyike? Sasa ni sheria gani nitatekelezwa bila kanuni? Kwahyo naishauri serikali iweke mpangilio mzuri wa kuwalinda na kuwasaidia walemavu sababu hatuna sehemu yoyote ya kujikita kama sio huko serikalini.
Read More ->>
 

| DISABILITY IN TANZANIA INFORMATION PLATFORM © 2012. All Rights Reserved |Designed by MIRAMBO GROUP | Back To Top |