Sunday, May 26, 2013

NALIA NA SERIKALI: ORAM CLIPHORD MAKARANGA

0 comments


Naitwa Oram Cliphord Makaranga, ni mwenyekiti wa chama cha albino wilaya ya Bunda. Nina ulemavu wa ngozi (albino) nilizaliwa hivi kwa mapenzi ya Mungu. Maisha yetu ni mabaya sana kwakweli maana hatuvumilii kukaa kwenye jua kabisa.

Jua limeisha nichomaa mpaka mwili wangu unazeeka sasa. Lakini namshukuru mkuu wa wilaya ya Bunda na mkuu wa mkoa wa Mara kwani wanatusimamia na kututetea na kutusaidia ingawaje sio viongozi wote wanaofanya hivo.
Changamoto yangu kubwa ni swala la afya, tunaumwa kwakweli. Kwamfano mimi ninasumbuliwa na saratani ya ngozi, namshukuru mkuu wa wilaya ya Bunda na mkuu wa mkoa wa Mara kwa kuweza kunisaidia na kunipa usafiri wa kunipeleka kwenye matibabu katika hospitali za Muhimbili na Ocean Road Dar es salaam. Lakini pamoja na hayo, mazingira tunayo ishi ni mabaya sana kwakweli, hatuna nyenzo za kutuwezesha kukaa kwenye kivuli muda wote.
Tunaiomba serikali ituthamini pamoja na kutupa misaada ya kila aina ili na sisi tujiskie kwamba hii nchi ni yetu na tunaishi salama. Wakati matamasha mbalimbali yanafanyika, kwa mfano siku ya walemavu kitaifa sisi hatuhusishwi kabisa, serikali inatutenga kabisa, wanakua kama hawatujui wala kututhamini. Hata kulala tunalala kwa shida, kusafiri kwa shida, kula kwa shida na tunataka tufike kwenye tamasha letu nasisi kama walemavu lakini kwakweli hawatuthamini. Nawaomba viongozi walioko madarakani watuthamini kama watu wengine.
Kinacho nisikitisha nikuona wazazi waliotuzaa wanatufukuza nyumbani nakutwambia twende kujitegemea. Tunaomba wazazi wetu watuthamini na kutupenda kama watu wa kawaida. Nilipopatwa na matatizo ya kansa nilichangiwa na marafiki zangu fedha za kunisaidia lakini wazazi wangu hawakunisaidia kabisa. Namwomba Mwenyezi Mungu awasaidie wawe na mapenzi na sisi, kwa mfano mimi nathaminiwa sana na watu wa nje kuliko wazazi wangu.
Read More ->>
 

| DISABILITY IN TANZANIA INFORMATION PLATFORM © 2012. All Rights Reserved |Designed by MIRAMBO GROUP | Back To Top |