Tuesday, September 17, 2013

TELEVISHENI KUTOKUA NA WAKALIMANI WA LUGHA ZA ALAMA NI UVUNJAJI WA SHERIA: DOLASED

0 comments



Mkurugenzi  Mtendaji  wa Taasisi ya isiyo ya kiserikali inayoshughulikia masuala ya haki  za kisheria ,maendeleo ya jamii na kiuchumi(DOLASED), Gidion Mandesi(kulia) akifafanua Sheria  ya Watu Wenye Ulemavu namba 55(1) ya mwaka 2010 na mtazamo wake juu vyombo vya habari hususani televisheni vinavyotakiwa kuweka wakalimani kwa ajili ya taarifa ya habari na matukio mengine ya kitaifa ili viziwi waweze kupata taarifa, kulia   ni mwandishi wa habari wa gazeti la majira , David John.


Picha kwa hisani ya Social Work Club.
 

Read More ->>

TUMEKUELEWA SANA RAPPER STAMINA KWA UJIO WA "KABWELA FOUNDATION"

0 comments


Usije kushangaa pale ambapo utamuona Rapper Stamina mtaani kwako akifanya shughuli za kijamii, kwasababu hivi sasa ameamua kuanzisha taasisi yake binafsi (NGO) aliyoipa jina la Kabwela Foundation.



"Ni Foundation ambayo nimeianzisha yaani ni kampuni kabisa ambayo tayari nimeshaisajili, na itakuwa inajihusisha zaidi na maswala ya kijamii, hasahasa kuwatembelea walemavu, maana kumekuwa na taaisisi nyingi ambazo zimekuwa zikiwaangalia sana watoto yatima, sasa mimi nitakuwa nikiwaangalia zaidi walemavu, sio yatima, kuna walemavu wana wazazi wao lakini hawajiwezi" alisema Stamina.
Aliongeza kwa kusema mpaka sasa tayari ameshapata atakaokuwa akishirikiana nao ambao ni wasanii wenzake, Young killer, G Warawara, Joe makini pamoja na Godzilla, ambapo atakuwa akitembelea kituo kimoja katika mkoa mmoja kila mwisho wa mwezi, na baada ya miezi 12 atakuwa ametembelea mikoa 12.

Umeeleweka sana!!! Jamii ya watu wenye ulemavu inakupongeza na kukuunga mkono katika juhudi zako.
Read More ->>
 

| DISABILITY IN TANZANIA INFORMATION PLATFORM © 2012. All Rights Reserved |Designed by MIRAMBO GROUP | Back To Top |