Sunday, February 17, 2013

Vishawishi vya wanajamii vilimfanya mume wangu anikimbie: PELESIANA JULIUS




Naitwa Pelesiana Julius natokea mji wa Bunda naishi katika mtaa wa mbugani. Nina umri wa miaka 36 na nina ulemavu wa viungo (natembea kwa kutambaa).

Mimi nilizaliwa nikiwa mzima na tulikua mapacha wawili, baadae mwenzangu akaugua na kufariki. Baada ya Kurwa kufariki basi ungonjwa ukawa umenishika mimi, niliugua kwa muda mrefu sana, mama angu akanizungusha mahosipitalini na kwa waganga mbalimbali matokeo yake miguu ikawa imepooza na ndo chanzo cha kupata ulemavu huu.
Kwasasahivi sina mume lakini kwa kipindi cha nyuma nilikua na mume aliye nizalisha watoto watatu (3), baadae akawa ameshawishika kwamba utaishije na mtu kiwete huwezi kutokanae hata matembezi? Akawa amekubaliana na hivyo vishawishi na kuondoka mwaka 2004 na kuniacha nahangaika na watoto. Namshukuru Mungu kwasasa wanangu wameishakua watu wazima na wanaweza kujihangaikia.
Maisha yanakua magumu kulingana na hali na shughuli ninazozifanya pia, unakuta shughuli zinakwama zinakua ngumu na watoto unao,pakukimbilia unakua huna. Hata ukikimbilia kwa ndugu, ni ndugu wachache wanaoweza kukusaidia, kila mtu atasema anaangalia mambo yake. Kwakweli nakua na shida nyingi sana nahangaika, hata sehemu za kuishi unaishi kwa shidashida. Nashukuru Mungu alinisaidia nikawa nimejenga kinyumba kidogo cha tope, lakini pia bado ninahangaika kwasababu nilipata kiwanja maeneo ya majimaji. Mvua zinapokuja nyingi zinanipa shida sana nahangaika, pamoja na hayo sina msaada wowote kusema mtu anaweza akanisaidia hata kwa kuniletea gari moja ya mawe ili ninyanyue nyumba iwe juu.
Naishauri serikali kwakweli itusaidie watu wenye ulemavu maan tunapata shida sana hasa swala la makazi na mazingira. Unaweza mtu ukawa unaishi nyumbani lakini unakuta choo kichafu, bafu chafu sasa jinsi ya kufanya usafi kwa mtu mwenye ulemavu inakua ni ngumu sana. Naiomba serikali itukumbuke sisi watu wenye ulemavu hata kama wale ambao Mungu ametusaidia tumepata sehemu za kujenga nyumba zetu wenyewe, serikali itusaidie hata kutuwezesha kujenga nyumba nzuri zenye vyoo vizuri vya kufikika ili nasisi tufurahie maisha.
Jamii naishauri imuangalie mtu mwenye ulemavu kama binaadamu wa kawaida kwasababu sehemu zingine tunaonekana kama watu wasio faa, inatakiwe watupe haki sawa kama watu wazima. Jamii isitunyanyase sababu ya ulemavu wetu. Walemavu wengi sana unakuta wametengwa sana. Unakuta mtu ni mchafumchafu tu. Sasa ule uchafu unakuta unatokana na kukosa msaada lakini sio kwamba jamii haiwezi kumsaidia ila wanaona kwakua ni mlemavu hana manufaa kwao. Tunahitaji jamii ituangalie kuwa nasisi ni watu.
Kwaupande wangu sipendi sana kulalamika, napia namshukuru Mungu kwasababu sipendi kukaa kwasababu eti ni mlemavu maana kama ni kulemaa nimelemaa miguu ila sijalemaa akili. Kwahyo ninacho washauri walemavu wenzangu nikwamba, kama mtu unao ulemavu unaokuruhusu kujishughulisha basi jishughulishe. Usije ukajiweka kwamba wewe ni mlemavu ukategemea jamii au serikali ikusaidie, kwa upande mwingine inakua ngumu. Pamoja nakwamba tunahitaji misaada kama watu wenye ulemavu lakini na sisi tunatakiwa tujipe nguvu ya kuweza kujisaidia wenyewe. Kwasababu mtu hata atakapokuona wewe unakua na kazi ya kufanya inayo weza kukupa kipato kidogo, unaweza ukakimbilia kwa mtu mwingine akakusaidia kulingana na kazi unayoifanya. Sasa ukiwa umekaa tu huwezi kukimbilia kwa mtu akukopeshe hata elfu tano (5000) akakubari sababu anajua huwezi kuipata kwa kukaa tu, lakini ukiwa unajishughulisha kama mlemavu unaweza kwenda sehemu ukakopa pesa pamoja nakwamba biashara kwetu zinakua ngumu kutokana na ufikikaji wa maeneo au kukosa msaada lakini inatubidi tushughulike kama watu wenye ulemavu. Serikali ijitahidi kutukumbuka jamani.

Kindly Bookmark this Post using your favorite Bookmarking service:
Technorati Digg This Stumble Stumble Facebook Twitter
YOUR ADSENSE CODE GOES HERE

0 comments:

Post a Comment

 

| DISABILITY IN TANZANIA INFORMATION PLATFORM © 2012. All Rights Reserved |Designed by MIRAMBO GROUP | Back To Top |