Thursday, May 9, 2013

ALBINO AFUKUZWA SHULE JIJINI MBEYA KWA MADAI KWAMBA NI MCHAWI




Amina Mwamkinga alisema tangu tarehe tisa alipofukuzwa bwenini na wanafunzi wenzie wakitaka aondoke shuleni hapo wakimtuhumu kuwa mchawi majira ya usiku hali iliyomlazimu kuomba hifadhi kwa mlinzi aliyemkubalia na kukesha naye hadi asubuhi  hali iliyopelekea kupigwa na baridi kali kutokana na kukosa nguo za kujisitiri kama Shuka nk.


Hapa Amina akimsimulia mkasa mzima mwandishi wa Mbeya yetu Joseph Mwaisango mara baada ya kupata maelezo yote ya Amina mwandishi alimpigia simu katibu wa chama cha maalbino mkoa wa Mbeya afike ofisi ya Mbeya yetu ili wasaidiane kutatua tatizo hilo.



katibu wa Chama cha Albino Mkoa wa Mbeya, Wiliamu Simwale akiwa makini kumsikiliza Amina katika ofisi ya Mbeya yetu


KATIKA Hali isiyokuwa ya Kawaida Uongozi wa Shule ya Sekondari Hollwood iliyoko Mlowo Wilayani Mbozi Mkoa wa Mbeya imemsimamisha shule Mwanafunzi wa kidato cha tatu kwa takribani Miezi Miwili kwa madai kuwa anajihusisha na imani za Kishirikina.
  
Mwanafunzi huyo aliyejulikana kwa jina la Amina Mwankinga(20) ambaye ni mlemavu wa ngozi(Albino) alisimamishwa shule na uongozi wa Shule hiyo tangu Machi 9, Mwaka huu baada ya uongozi wa Shule hiyo kupata taarifa kutoka kwa Wanafunzi wakimtuhumu Mwenzao huyo kuwa ni Mshirikina.
  
Uongozi wa Shule hiyo baada ya kupata taarifa hizo ulimwamuru mhanga wa tukio hilo kuondoka Shuleni hapo pasipo kufuatilia na kujua ukweli wa jambo hilo na kupata udhibiti hivyo kumwacha Mwanafunzi huyo akizurura mitaani asijue hatma ya maisha yake.
  
Mhanga wa tukio hilo Amina Mwankinga alisema tangu tarehe tisa alipofukuzwa bwenini na wanafunzi wenzie wakitaka aondoke shuleni hapo majira ya usiku hali iliyomlazimu kuomba hifadhi kwa mlinzi aliyemkubalia na kukesha naye hadi asubuhi  hali iliyopelekea kupigwa na baridi kali kutokana na kukosa nguo za kujisitiri kama Shuka nk.

Anasema kutokana na hali hiyo Walimu pamoja na uongozi wa Shule hiyo haukuchukua hatua yoyote jambo lililomlazimu kuondoka Shuleni hapo  baada ya kukosa msaada ambapo alirejea Jijini Mbeya anakoishi na Binamu yake.
  
Binti huyo anayesomeshwa na Shirika la Under the SameSun  iliyoko Jijini Dar Es Salaam aliwaambia waandishi wa habari kuhusu mkasa uliompata huku akiomba msaada kwa wasamaria wema kumtafutia Shule ili aendelee na masomo kwa ajili ya kujiandaa na mtihani wa kidato cha nne Mwakani.
  
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya HollyWood Ambukeghe Mtafya, alipopigiwa simu kuhusu tuhumahizo alikiri kulijua suala hilo na kwamba walimrudisha mwanafunzi huyo nyumbani ili kumnusuru na kipigo kutoka kwa wanafunzi wenzie na kuongeza kuwa aliambiwa atafute shule nyingine ili ahamie.
  
Naye katibu wa Chama cha Albino Mkoa wa Mbeya, Wiliamu Simwale  alisema alikuwa  halijui suala hilo na kwamba kama lingekuwa suala liko nyeti angejulishwa yeye juu ya hatua zilizofikiwa ambapo Uongozi wa Shule umeendelea kupokea fedha za malipo ya Mwanafunzi pasipo kutoa taarifa kwenye shirika linalolipa.
Mlezi wa Wanafunzi hao kutoka Shirika la Under the Samesun Omary Mfaume amesema kwamba hana taarifa zozote  kuhusiana na tukio hilo na kuongeza kuwa anawasiliana na uongozi wa Shule moja kwa moja ili umweleze juu ya kilichotokea ili taratibu za kumtafutia Shule nyingine zifanyika haraka ili Mwanafunzi aendelee na masomo kama kawaida.

Na Mbeya yetu. 
 

 

Kindly Bookmark this Post using your favorite Bookmarking service:
Technorati Digg This Stumble Stumble Facebook Twitter
YOUR ADSENSE CODE GOES HERE

0 comments:

Post a Comment

 

| DISABILITY IN TANZANIA INFORMATION PLATFORM © 2012. All Rights Reserved |Designed by MIRAMBO GROUP | Back To Top |