RISALA YA SHIVYAWATA, VYAMA VYAKE, NA VYAMA VYA HUDUMA
KWA WATU WENYE ULEMAVU KWA MGENI RASMI, WAZIRI
MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MHESHIMIWA MIZENGO KAYANZA PETER PINDA KWENYE MAADHIMISHO YA SIKU YA WATU WENYE
ULEMAVU DUNIANI LEO TAREHE 3 DESEMBA 2012 – MARA MUSOMA.
Mheshimiwa
Mgeni Rasmi- Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Mh. Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii
Mh.
Kamishna – Idara ya Ustawi wa Jamii,
Mh.
Mkuu wa Mkoa wa Mara;
Weheshimwa
Wakuu wa wilaya, Wakurugenzi na viongozi wengine wote wa Serikali kwa vyadhifa
zenu
Waheshimiwa
Viongozi wa Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania
Waheshimiwa
wadau wa Masuala ya Watu Wenye Ulemavu
Wajumbe
wa Kamati ya Maandalizi ya Musoma na Dar es Salaam
Waheshimiwa
viongozi wa vyama vya siasa,
Waandishi
wa Habari ,
Ndugu
wageni waalikwa; Mabibi na mabwana itifaki imezingatiwa.
Awali
ya yote napenda kutumia nafasi hii kumshukuru
Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kuifikia siku hii
muhimu kwa watu wenye ulemavu Duniani.
Aidha,
tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwako Mgeni Rasmi kwa kukubali mwaliko
wetu na kuja kujumuika nasi katika kuadhimisha
siku hii muhimu ya watu wenye ulemavu nchini na duniani kwa kote.
Tunafahamu
kuwa una majukumu mengi ya Kitaifa na Kimataifa, kukubali kwako mwaliko wetu ni
uthibitisho wa wazi kwa Watanzania, kuwa wewe ni mtu wa watu na unayewajali
Watanzania bila kujali tofauti zao.
Mheshimiwa Mgeni Rasmi, Shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania
kwa kushirikiana na wadau wa masuala ya watu wenye ulemavu wote hapa nchini tumekuwa
tunaadhimisha siku hii kila mwaka tangu kutolewa tamko la Baraza la Umoja wa
Mataifa katika Azimio No. 47/3 la 1992. Lengo la maadhimisho haya ni
kuhamasisha jamii, serikali pamoja na wadau katika sekta mbalimbali kutambua uwezo
na mchango wa watu wenye ulemavu, Ikiwa ni pamoja mchangamoto zinazowakabili
ili kujenga mazingira yanayotoa fursa sawa katika ushiriki wao kwenye shughuli
za maendeleo katika Nyanja mbalimbali za jamii.
Mheshimiwa Mgeni
Rasmi, mwaka huu
2012 ambao ni mwaka wa ishirini wa maadhimisho haya hapa nchini umebebwa na
kauli Mbiu “ONDOSHA VIKWAZO ILI KUJENGA JAMII
JUMUISHI INAYOFIKIKA KWA WOTE”
Mheshimiwa Mgeni
Rasmi, katika
maadhimisho haya tunapenda jamii itambue vikwazo anavyokabiliana navyo mtu
mwenye ulemavu, ili ishiriki kwa dhati katika kuviondoa na kumwezesha mtu
mwenye ulemavu ashiriki kikamilifu katika shughuli mbalimbali za maendeleo
ikiwa ni pamoja na kuzifikia huduma zote za kijamii.
Mheshimiwa mgeni
rasmi, katika
safari ndefu ya kudai huduma rafiki kwa watu wenye ulemavu kutambuliwa,
kuthaminiwa pamoja na kuheshimu utu wa mtu mwenye ulemavu, tunapenda kuishukuru
sana serikali kwa yafuatayo:-
-
Kuandaa
sera ya Maendeleo ya watu wenye ulemavu ya 2004
-
Kutambuliwa
kwa watu wenye ulemavu katika MKUKUTA
-
Kuwezesha
kuongezeka kwa idadi ya watu wenye ulemavu wanaopata elimu kuanzia shule ya
msingi hadi Elimu ya Juu
-
Kusaini
na kuridhi Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Haki za watu wenye ulemavu wa 2006.
-
Kupitisha
sheria Na.9 ya haki za watu wenye ya 2010
-
Kuwezesha
watu wenye ulemavu angalau kushiriki na kuadhimisha siku za watu wenye ulemavu
kupitia Bajeti za Halmashauri
-
Kusambazwa
kwa waraka wa serikali kote nchini kupitia TAMISEMI unaoelekeza utekelezaji wa
utoaji wa matibabu bure kwa watu wenye ulemavu katika hospitali zote za umma na
kuzuia kufukuzwa watoto wenye ulemavu pindi wanapokosa ada kuanzia July, 2012.
-
Kuendelea
kupata ondoleo la kodi kwa vifaa vya watu wenye ulemavu vinavyoingizwa nchini
kama msaada kwa matumizi ya watanzania wasio na uwezo wa kununua vifaa hivi
ambavyo ni aghali sana kwa mtu mwenye kipato cha chini.
Mheshimiwa Mgeni
Rasmi,
Pamoja na masuala yote tuliyoeleza
hapo juu, bado kuna changamoto kadhaa zinazotukabili watu wenye Ulemavu ambazo imekuwa
vikwazo kwa watu wenye ulemavu kufikia huduma za jamii pamoja na kuweza
kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo hizi ni pamoja na:-
-
Upatikanaji
wa taarifa muhimu katika mifumo isiyorafiki kwa watu wenye ulemavu. Viziwi
wamekuwa wakikosa taarifa muhimu zinazotangazwa kupitia Luninga kutokana na
kutokuwepo wakalimani wa lugha ya alama. Hivyo kuwafanya wakose kufuatilia
taarifa muhimu kama Hotuba za Rais kila mwezi, mijadala ya kielimu, taarifa za
habari na vipindi vya Bunge
-
Miundo
mbinu isiyo rafiki kwa watu wenye ulemavu, majengo mengi yanayotoa huduma kwa
umma hayafikiki na watu wenye ulemavu hii ikiwemo ofisi inayoratibu masuala ya
watu wenye ulemavu.
-
Kukosekana
kwa alama maalumu za barabarani ambazo zingewawezesha madereva na watu wengine
kuziheshimu ili watu wenye ulemavu kumudu kutumia barabara kwa uhuru. Vile vile
vyombo vya usafiri kama mabasi, traini na vyombo vya majini pamoja na viwanja
vyote vya ndege si rafiki kwa watu wenye ulemavu kwa kukosa nyenzo muhimu na
nafasi maalumu kwa watu wenye ulemavu wanapotumia vyombo hivi.
-
Ruzuku
ndogo kwa vyama vya watu wenye ulemavu isiyokidhi mahitaji ya msingi katika
kutoa huduma kwa watu wenye ulemavu na isiyotolewa kwa wakati, na miaka mingine
kupita bila kupatiwa.
-
Kukosekana
kwa uwakilishi wa watu wenye ulemavu katika vyombo vingi vya maamuzi kuanzia ngazi
za serikali za mitaa hadi serikali kuu, hii ni kwa vile
si wote katika vyombo hivi wenye ujuzi juu ya mahitaji halisi ya watu wenye
ulemavu, hivyo kupelekea mipango mingi ya maendeleo kutokuzingatia mahitaji ya
watu wenye ulemavu.
-
Kukosekana
kwa ofisi ya kudumu kwa Shirikisho la Vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania
ambalo limekuwa kiunganishi baina ya vyama vya watu wenye ulemavu, taasisi
zinazohudumia watu wenye ulemavu, Serikali na wadau mbalimbali
Mheshimiwa Mgeni Rasmi,
kutokana na changamoto
tulizozibainisha hapo juu, SHIVYAWATA na wadau wa masuala ya watu wenye
ulemavu tunapendekeza yafuatayo kwa Serikali na kupitia kwako Mgeni Rasmi,
-
Katika
kukabili kikwazo cha upatikanaji wa habari, Serikali ihimize uwepo wa wakalimani
wa lugha ya alama katika vyombo vya habari kila inapotolewa taarifa muhimu kwa
umma. Na kwa kuanzia walau iwezeshe uwepo wa Wakalimani katika Television ya
Taifa, vikao vyote vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na
Hotuba za Mh. Rais za kila mwezi kwaajili ya
viziwi kupata habari. Pia iwezeshe uchapaji wa nyaraka muhimu kama sera, sheria
na mipango mikakati ya serikali na miongozo mbali mbali ya kazi kwa maandishi
ya nukta nundu na maandishi yaliyokuzwa ili kutoa fursa kwa wasioona na wale
wenye uoni hafifu kuweza kuzifahamu na kuzitumia ipasavyo .
-
Tunaiomba
Serikali kupitia SUMATRA ihakikishe vyombo vyote vya usafiri kwa umma kama vile
mabasi, daladala, treini na meli vinavyoagizwa vinakidhi viwango vya ufikikaji
kwa watu wenye ulemavu.
-
Tunaiomba
Serikali ihakikishe kuwa ujenzi wa viwanya vya ndege, majengo ya umma chini ya
NSSF, NHC, TBA na mamlaka nyingine pamoja na barabara unaoendelea hapa nchini
hususani kwenye miji, miundo mbinu yake ikidhi viwango vya ufikikaji kwa watu
wote wenye ulemavu.
-
Serikali
iwezeshe vyuo vya Mafunzo kwa watu wenye ulemavu vilivyo chini ya Idara ya
ustawi wa jamii ambavyo vimefungwa kufufuliwa, ili kuwapa ujuzi watu wenye
ulemavu waweze kuishi maisha ya kujitegemea
-
Serikali,
izielekeze na kuziwezesha Mamlaka za Elimu na Ufundi (VETA), SIDO na Chuo cha
Uhandisi cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,
kufanya utafiti na kuanza kutengeneza vifaa vya kujimudu kwa watu wenye
ulemavu kama fimbo nyeupe, baiskeli na pikipiki za miguu mitatu hapa nchini ili
kukabili ughali wa nyenzo hizo muhimu kwa wenye ulemavu.
-
Serikali
ikamilishe Uchapaji wa Kanuni za sheria ya watu wenye ulemavu kama ambavyo
imeahadi mara kadhaa ili kuwezesha utekelezaji wa sheria ya watu wenye ulemavu
ya 2010
-
Serikali
ikamilishe uundwaji wa Baraza la watu wenye ulemavu ili kuwezesha ufanisi
katika utekelezaji wa Sheria ya watu wenye ulemavu iliyoanza kufanya kazi rasmi
2010.
-
Serikali
iwezeshe upatikanaji wa Ofisi ya kudumu ya Shirikisho la Vyama vya Watu wenye
Ulemavu nchini (SHIVYAWATA) ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea pindi
wafadhili wa nje watakapositisha ufadhili wa pango la Ofisi (katika hili
tunapenda kukumbushia ahadi yako iliyoitoa 2008 tulipokutembela nyumbani kwako
Dodoma) bado tungali tunasubiria.
Ndugu Mgeni rasmi, kwa mara nyingine tunaomba Serikali
iafiki kuhamishia uratibu wa maswala ya watu wenye Ulemavu katika Wizara yenye
mamlaka juu ya Wizara nyingine, kama vile Ofisi ya Waziri Mkuu au Ofisi ya
Rais. Hiki kilio chetu kinatokana na kwamba Idara inayoratibu kwa sasa haiwezi
kuagiza wizara nyingine kujumuisha na kutekeleza upatikanaji wa mahitaji ya
watu wenye ulemavu katika mipango yao. Katika hili bado tunakumbuka nia yako ya
dhati ya kutekeleza hili japo hatujui lilikwama wapi.
Ndugu Mgeni Rasmi, SHIVYAWATA na wadau wote haki za
watu wenye ulemavu tunatambua na kuthamini azma ya serikali kuanzisha na
kusimamia mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya ya nchi baada ya miaka 50 ya
uhuru. Fursa hii ni muhimu katika kuhakikisha kuwa jamii inazingatia haki na
usawa miongoni mwa makundi yote hapa nchini. Hivyo tunaiomba serikali
ihakikishe kuwa sauti za watu wenye ulemavu kuhusu haki na mahitaji yao
yanazingatiwa kikamilifu katika katiba mpya ijayo. Watu wenye ulemavu tunaamini
kuwa vikwazo vitapata ufumbuzi tu endapo katiba ya nchi itatambua bayana haki
na mahitaji yatu.
Mwisho Mheshimiwa
Mgeni Rasmi, tunaomba
kutumia nafasi hii kuwashukuru marafiki na wadau wa masuala ya watu wenye
ulemavu ambao wamechangia kwa namna moja au nyingine katika kufanikisha
maadhimisho haya. Aidha, tunapenda kukushukuru tena wewe binafsi Mh. Mgeni
Rasmi na wageni waalikwa wote kwa kujumuika nasi leo tukiamini kuwa serikali
itasikia kilio cha watu wenye ulemavu.
Ahsante
…………………….
Lupi Maswanya
Mwenyekiti-SHIVYAWATA
Read More ->>