Naitwa Pelesiana Julius natokea mji wa Bunda
naishi katika mtaa wa mbugani. Nina umri wa miaka 36 na nina ulemavu wa viungo
(natembea kwa kutambaa).
Mimi nilizaliwa nikiwa mzima na tulikua mapacha
wawili, baadae mwenzangu akaugua na kufariki. Baada ya Kurwa kufariki basi
ungonjwa ukawa umenishika mimi, niliugua kwa muda mrefu sana, mama angu
akanizungusha mahosipitalini na kwa waganga mbalimbali matokeo yake miguu ikawa
imepooza na ndo chanzo cha kupata ulemavu huu.
Kwasasahivi sina mume lakini kwa kipindi cha nyuma nilikua na mume aliye
nizalisha watoto watatu (3), baadae akawa ameshawishika kwamba utaishije na mtu
kiwete huwezi kutokanae hata matembezi? Akawa amekubaliana na hivyo vishawishi
na kuondoka mwaka 2004 na kuniacha nahangaika na watoto. Namshukuru Mungu
kwasasa wanangu wameishakua watu wazima na wanaweza kujihangaikia.
Maisha yanakua magumu kulingana na hali na
shughuli ninazozifanya pia, unakuta shughuli zinakwama zinakua ngumu na watoto
unao,pakukimbilia unakua huna. Hata ukikimbilia kwa ndugu, ni ndugu wachache
wanaoweza kukusaidia, kila mtu atasema anaangalia mambo yake. Kwakweli nakua na
shida nyingi sana nahangaika, hata sehemu za kuishi unaishi kwa shidashida.
Nashukuru Mungu alinisaidia nikawa nimejenga kinyumba kidogo cha tope, lakini pia
bado ninahangaika kwasababu nilipata kiwanja maeneo ya majimaji. Mvua
zinapokuja nyingi zinanipa shida sana nahangaika, pamoja na hayo sina msaada
wowote kusema mtu anaweza akanisaidia hata kwa kuniletea gari moja ya mawe ili
ninyanyue nyumba iwe juu.
Naishauri serikali kwakweli itusaidie watu
wenye ulemavu maan tunapata shida sana hasa swala la makazi na mazingira.
Unaweza mtu ukawa unaishi nyumbani lakini unakuta choo kichafu, bafu chafu sasa
jinsi ya kufanya usafi kwa mtu mwenye ulemavu inakua ni ngumu sana. Naiomba
serikali itukumbuke sisi watu wenye ulemavu hata kama wale ambao Mungu
ametusaidia tumepata sehemu za kujenga nyumba zetu wenyewe, serikali itusaidie
hata kutuwezesha kujenga nyumba nzuri zenye vyoo vizuri vya kufikika ili nasisi
tufurahie maisha.
Jamii naishauri imuangalie mtu mwenye ulemavu
kama binaadamu wa kawaida kwasababu sehemu zingine tunaonekana kama watu wasio
faa, inatakiwe watupe haki sawa kama watu wazima. Jamii isitunyanyase sababu ya
ulemavu wetu. Walemavu wengi sana unakuta wametengwa sana. Unakuta mtu ni
mchafumchafu tu. Sasa ule uchafu unakuta unatokana na kukosa msaada lakini sio
kwamba jamii haiwezi kumsaidia ila wanaona kwakua ni mlemavu hana manufaa kwao.
Tunahitaji jamii ituangalie kuwa nasisi ni watu.
Kwaupande wangu sipendi sana kulalamika, napia namshukuru Mungu
kwasababu sipendi kukaa kwasababu eti ni mlemavu maana kama ni kulemaa
nimelemaa miguu ila sijalemaa akili. Kwahyo ninacho washauri walemavu wenzangu
nikwamba, kama mtu unao ulemavu unaokuruhusu kujishughulisha basi
jishughulishe.
Usije ukajiweka kwamba wewe ni mlemavu ukategemea jamii au serikali ikusaidie,
kwa upande mwingine inakua ngumu. Pamoja nakwamba tunahitaji misaada kama watu
wenye ulemavu lakini na sisi tunatakiwa tujipe nguvu ya kuweza kujisaidia wenyewe.
Kwasababu mtu hata atakapokuona wewe unakua na kazi ya kufanya inayo weza
kukupa kipato kidogo, unaweza ukakimbilia kwa mtu mwingine akakusaidia
kulingana na kazi unayoifanya. Sasa ukiwa umekaa tu huwezi kukimbilia kwa mtu
akukopeshe hata elfu tano (5000) akakubari sababu anajua huwezi kuipata kwa
kukaa tu, lakini ukiwa unajishughulisha kama mlemavu unaweza kwenda sehemu
ukakopa pesa pamoja nakwamba biashara kwetu zinakua ngumu kutokana na ufikikaji
wa maeneo au kukosa msaada lakini inatubidi tushughulike kama watu wenye
ulemavu. Serikali ijitahidi kutukumbuka jamani.
Read More ->>