Monday, March 4, 2013

‘Kutokua na fursa katika mambo mbalimbali kinaweza kua ni kichocheo kingine cha kutufanya tusikubalike katika jamii.’ YOHANA CHACHA

2 comments


YOHANA CHACHA
Naitwa Yohana Chacha ni mkazi wa wilaya ya Butiama, kijiji cha Makutano. Mimi sina familia kutokana na halingumu ya kiuchumi na mzaingira tunayoishi. Nina ulemavu wa macho na nilizaliwa nikiwa na hali hiitangu tumboni mwa mama. 

Kwakipindi kilichopita nilikua nafanya biashara ndogondogo (kioski) ila kutokana na matatizo ya hapa na pale mtaji wangu ukawa umeisha na sasahivi sina kazi kabisa.
Changamoto ninazo kumbana nazo ni kwa upande wa jamii inayotuzunguka kutokutukubali kama binaadamu kamili. Nashindwa kuelewa chanzo cha tatizo hili, sijui ni elimu ndogo ama nini?. Unajua kwa huku kwetu vijijini swala la elimu kwa jamii nikama halipo, kwahiyo wanatuchukulia sisi walemavu kama watu tulioumbwa kwa bahati mbaya au matunda ya laana.
Kutokua na fursa katika mambo mbalimbali kinaweza kua ni kichocheo kingine cha kutufanya tusikubalike katika jamii. Jamii inatuchukulia kama mzigo, hata lile ambalo ungewezeshwa ukaweza linakua ni vigumu kwa mlemavu kuwezeshwa. Namshukuru Mungu kuona mpaka leo bado nipo pamoja na mambo mengimengi niliyo kumbananayo.
Kinachotakiwa kwa jamii, ingefaa kwanza vyombo vya habari (radio, TV, pamoja an magazeti) waweze kutoa elimu kwa jamii za watu walio vijijini juu ya namna na jinsi ya kuishi na kuwathamini watu wenye ulemavu kama watu wengine. Wasitudharau, kutunyanyapaa, kutukejeli wala kututenga. Wafute mitazamo hasi waliyonayo dhidi yetu sisi watu wenye ulemavu.
Nawashauri wenzangu wenye ulemavu yakwamba tufanye ushirikiano na kutengeneza sauti ya pamoja, ili kuwaeleza jamii inayotuzunguka kwamba nasisi tunahaki na tunastahili heshima zote. Pamoja nakwamba tuna ulemavu lakini tuifanye jamii itambue kwamba hata sisi tunaweza tukatoa mawazo yakasikilizwa na tunaweza tukafanya kitu kikaonekana. Tusiwe watu tegemezi kila wakati.
Naishauri serikali isaidie katika kuielimisha jamii kuhusu maswala ya watu wenye ulemavu. Msisitizo mkubwa uwekwe kwa jamii za wanaoishi vijijini na isiishie tu mijini kama ilivo sasa. Ukizunguka katika vijiji utakuta kuna walemavu ambao hawapewi fursa yoyote, hata mgeni akifika nyumbani utakuta mlemavu anafichwa ndani. Mimi kunakipindi hali hiyo ilinikuta lakini nilipambana nayo. Serikali izunguke na kuwahamasisha wazazi wenye watoto walemavu kuwapeleka watoto wao shule. Serikali isiishie kutoa mikopo ya biashara kwa watu wazima peke yao, itambue pia kua kuna jamii ya watu wenye ulemavu ambayo ili iondokane na hali ya kuitwa ombaomba. Wakiwezeshwa wakapewa mikopo yenye masharti nafuu wanaweza kufanya kitu kinachoonekana napia wakachangia katika kulipa kodi pia.
Read More ->>
 

| DISABILITY IN TANZANIA INFORMATION PLATFORM © 2012. All Rights Reserved |Designed by MIRAMBO GROUP | Back To Top |