HAKI ZA BINADAMU NA ULEMAVU KIKATIBAKUTANZUA ULEMAVU KUPITIA MCHAKATO WA KATIBA YA ZAMANI NA KUINGIZA KATIKA KATIBA MPYA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KUTANZUA ULEMAVU KUPITIA MCHAKATO WA
KATIBA YA ZAMANI NA KUINGIZA KATIKA KATIBA (SOLUTIONS ON DISABILITY
BARRIERS)
HAKI ZA BINADAMU KWA
WATU WENYE ULEMAVU KIKATIBA
Utangulizi
Kwa muda mrefu sasa watu wenye ulemavu
(wwu) nchini wamekuwa wakinyanyaswa na
kunyimwa haki zao za ajira, elimu, afya na utengamao wa maisha yao. Mfumo wa
sheria umechelewa sana kwani baada ya miaka 50 tangu kupata uhuru watu wenye
ulemavu ndiyo wamefanikiwa kushawishi kutungwa kwa sheria namba 9 ya 2010
inayohusu Haki na ulinzi kwa watu wenye
ulemavu (WWU)Tanzania.
Haki za watu wenye ulemavu zinatokana
na msingi wa kikatiba kama ilivyo makundi mengine katika jamii. Kipengele cha Haki ya usawa, Ibara ya 13 ya katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inakataza aina zote za ubaguzi,
yaani ubaguzi wa rangi, utaifa, Jinsia,
na hali nyinginezo yaani ikiwemo na kundi la watu wenye ulemavu.
Pia matamko mbalimbali ya Umoja wa
mataifa yatambua kuwepo kwa kundi hili la ,hasusani watu wenye ulemavu.Tamko la Haki za binadamu la mwaka 1948,
na kanuni za fursa sawa na haki kwa WWU za Umoja wa Mataifa na mkataba wa
kimataifa wa ulinzi wa haki na hadhi kwa WWU tamko hili linajulikana kama ‘’ Mkataba wa kimataifa wa kulinda Haki na Hadhi za watu wenye ulemavu’’.
Na mnamo tarehe 24.04.2009 bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania liridhia
mkataba huo, kitendo ambacho kimesababisha mkataba huu kutumika nchini kama
mojawapo ya nyenzo ya kutungwa kwa Sheria namba 9 ya mwaka 2010 inayohusu Haki
na ulinzi kwa watu wenye ulemavu Tanzania.
Falsafa ya Ulemavu
Kihistoria
watu wenye ulemavu kwa muda mrefu sana wamekumbwa na vikwazo vya aina nyingi,
na kikubwa kuliko yote ni ile hali ya unyanyapaa.katika jamii za kale kila
mwanajamii alikuwa na wajibu wa kutoa
mchango fulani katika uzalishaji mali na utafutaji chakula.
Mtu
anapotokea kupoteza moja ya viungo vyake, ni wazi kwamba atashindwa
kushiriki kikamilifu katika harakati za uzalishaji mali hasa
kipindi hicho cha kale ambapo sayansi na tenkolojia ilikuwa duni hivyo basi matokeo yake tamaduni zetu za
kiafrika zinaufananisha ulemavu na mambo
kama vile adhabu, laana, mkosi ndio maana baadhi ya makabila yaliwaua ,
kuwatupa kuwatekeleza na kuwaficha majumbani mwao kwa kuhofia aibu.
Huu ndio
msingi mkubwa unaosababisha hata watunga sera
zetu wakawa na mtazamo wa namna hii. Wataalamu wa mambo ya watu wenye ulemavu wanawagawa makundi ya jamii
sehemu tatu kama ifuatavyo;
Kundi
la kwanza: Mbinu ya makundi ya hisani;
Ni yale tu
ambayo yanamshughulikia au kumsaidia mtu mwenye ulemavu kwa sababu ya hofu ya
Mungu na siyo kwa kujali utu wa huyo mhusika, kutoa vihela vichache, chakula,
tafrija, wakiamini kwamba watapata
thawabu kwa muumba wao.
Kundi la pili: Mbinu /mtazamo wa tiba;
Ni watu ambao
wanaona kwamba mtu mwenye ulemavu ni sawa na mgonjwa anayehitaji kutibiwa,
hivyo basi hufanya harakati nyingi ili kuhakikisha kwamba, hali ya mtu mwenye
ulemavu inakuwa bora kwa kumkarabati na kujaribu kumrudisha katika hali yake ya
awali.
Kundi hili ni
la hatari pia kwa sababu wakati mwingine limekuwa likibuni mbinu za kisayansi
kama vile kuharibu mimba ambayo wanadhani kwamba mtoto atakayezaliwa atakuwa mtoto
ni mtoto mwenye ulemavu au kumwangamiza mara tu atakapozaliwa na ulemavu hasa
wakifahamu kwamba hawezi kufanyiwa ukarabati wa aina yoyote.
Kwa upande wa Viziwi kundi hili linakarabati
masikio kwa kuweka vitu mbadala ili kulazimisha Kiziwi asikie kwa kutumia vifaa
hivyo (Cholera Implant).
Kwa kufanya hivyo kuna matokeo zaidi ya kuwa
Kiziwi, kwani katika kukarabati wakati mwingine Kiziwi anapooza au kupinda kwa
baadhi ya viungo kama vile mdomo, taya, na macho. Anakuwa Kiziwi na kuongezewa
ulemavu mwingine.
Kundi la pili: Mbinu /mtazamo wa Kijamii;
Kundi hili ni
lililohamasika. Hili hutanguliza utu wa mhusika kabla ya kufikiria udhaifu
wake. Lengo la kundi hili ni kuvitumia vipaji vingine alivyo navyo MMU na kumpa
elimu, nyenzo na mbinu mbalimbali na kumwezesha mtu huyo kuchangamanika na
jamii na kujiletea maisha bora kama wanajamii wengine. Kundi hili ndilo
linaungwa mkono na wanaharakati wa WWU duniani kote.
KUTANZUA VIKWAZO KWA WATU WENYE ULEMAVU NCHINI TANZANIA
Vikwazo kwa watu
wenye ulemavu Duniani vinafanana na ni
vingi, lakini wanaharakati wa haki za watu wenye ulemavu (WWU) wanavigawa
katika makundi matatu kama ifuatavyo;
Kikwazo cha Kimtazamo hasi/Attitudinal
Huu ni ubaguzi wa kijamii kwa WWU kwa
kutafsiri au kuangalia ulemavu katika hali hasi, ni balaa, mkosi
laana na aibu. Hili linawakuta wote, WWU na jamii. Ni suala la ujinga kuhusu
visababishi vya ulemavu na kukata tamaa juu ya kile wanachomudu kufanya au
kutelekeleza WWU katika jamii mfano;
1. Tumeamua kuwa huwezi/Je, unataka sisi
tukulipie matibabu “ Hongera sana” (We
have decided you can not, Do you want us to pay for your treatment, ‘’Very
brave’’)
2.
Sawa, sihitaji msaada…, Maskini mwanangu – (Its ok
I don’t need help, Poor child)
3. Ni bora ufanye kazi mahali penye
kelele, Haitakudhuru kitu… (Good to work in noisy place, Can not expect to…)
Je,
tufanyeje? Katiba ya Tanzania itanzue kikwazo hiki kwa kutamka kwamba…
Kikwazo
cha Kimazingira/ The barrier of Environmental
Ni ubaguzi wa hali ya kuwatenga watu
wenye ulemavu pale majengo ya umma au yale yatoayo huduma kwa umma, vyombo vya
usafiri, bidhaa na huduma mbalimbali, vinaposanifiwa, kujengwa au kutolewa bila
kutilia maanani mahitaji maalum ya WWU, mathalani wale wenye tatizo la
ujongeaji, mfano;
1.
Maji/
Visima/ bomba- Water/well/Tap, Public buildings,Washrooms, Homes
2.
Michezo/Burudani/mawasiliano
na shule/ Sports/Leisure, Communications, School
3.
Vigumu
kupanda cheo,Vituao vya afya, na usafiri/ Difficult for promotion, Health
centers,Transport etc.
Je,
tufanyeje? Katiba ya Tanzania itanzue kikwazo hiki kwa kutamka kwamba…
1. Miundo mbinu yote ya umma, mfano
majengo, vyombo vya usafiri, barabara, njia, iwe vinafikika, vinaendeshwa na inatumika bila kikwazo kwa kila mtu na kwa
wakati wote.
2. Lugha za Taifa za Mawasiliano ni Kiswahili, Kiingereza, Lugha ya alama (katika kuwasiliana na wenye
ulemavu kiziwi), Maandishi ya nukta nundu (katika kuwasiliana wenye ulemavu wa
kutoona) Kila sehemu inayotumika na umma kuwepo na uwezeshaji wa lugha hizi
kikamilifu.
Kikwazo cha kisera na
kisheria/Institutional
Ubaguzi huu umekuwa ikitokea duniani
kwa kudhamiria au kutodhamiria hadi miaka ya hivi karibuni. Ndiyo maana kuna makundi
ya raia yanayoitwa ya pembezoni miongoni mwao wakiwemo WWU. Kubaguliwa huku
kumechangiwa sana na makundi husika kutokuwa na sauti ya pamoja katika
uhamasishaji, uraghibishi na utetezi.
Kulihibuka na wanaharakati wenye fikra
za kimapinduzi za kitafiti na kugundua na kutegua kitendawili cha ulemavu kwa
kutofautisha na neno ki/vilema. Na kuwa ‘’Kilema
chake siyo tatizo, bali jamii iliyomzunguka’’
Ubaguzi huu unatokea pale sheria,
kanuni au miongozo, sera au mipango ya maendeleo inaposhindwa kutaja bayana ni
kwa jinsi gani watu wenye ulemavu watanufaika.
Ukimya huu, huwafanya wahusika ndani ya kundi hili kwa namna moja au
nyingine waonekane raia daraja la pili wasio na haki ya kupata fursa ya
kujiendeleza kihali na kiakili kama vile kupata elimu, kuajiriwa, masuala ya
siasa, kujiwakilisha kwenye vyombo ya utungaji sera, kufanya maamuzi ngazi
mbali mbali na kuzaa na kulea watoto nk. Mfano;
1.
Imani
potofu, haiwezekani kugombea au kupiga kura au kuwakilishwa, wakilisha –
( Tradition, Can not stand for election
or representation, No vote).
2.
Hakuna
kufunga ndoa, ajira, hakuna haki ya kuwa na ardhi- ( No marriage,employment, No
land rights)
3.
Masuala
ya uchumi, mfano benki mikopo au mikataba- (Bank/credit/Loan, formal contracts)
Je,
tufanyeje? Katiba ya Tanzania itanzue kikwazo hiki kwa kutamka kwamba…
1. Mamlaka mahsusi ya nchi au Baraza kama
ilivyotajwa katika sheria ya mwaka 2010 ya itawekwa chini ya ofisi ya Ofisi ya Rais au Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ili
kuratibu kimantiki na kuhakikisha kwamba sera ya mwaka 2004 inaboreshwa zaidi,
inakidhi makundi tofauti tofauti ya watu wenye ulemavu na vyama vyote
vilivyosajiriwa kihalali kisheria katika mamlaka zote za usajili kuanzia ngazi
ya Taifa, vinajumuishwa katika mamlaka hiyo. Vile ile kila Wizara na taasisi
zake zitakuwa na dawati linaloshughulikia masuala ya wwu.
2. Mamlaka mahsusi ya nchi au Baraza kama
ilivyotajwa katika sheria ya mwaka 2010 inaratibu kimantiki na kuhakikisha
kwamba Mkataba wa kimataifa wa kulinda Haki na Hadhi za watu wenye ulemavu’’ Na
Sheria namba 9 ya mwaka 2010 inayohusu Haki na ulinzi kwa watu wenye ulemavu
Tanzania inatekelezwa kwa kufuata wakati na kutoa mrejesho unaotakiwa
kikamilifu.
1. Watu wenye ulemavu wawe na nafasi maalum
za uwakilishi, kulingana na uanisho la makundi
ya ulemavu kama vile wenye ulemavu
wa viungo, wasioona, Albino, Viziwi, Viziwiwasioona, Uti wa mgongo,
Akili, Kupooza, na ulemavu mwingine mchanganyiko, pia kutakuwepo na wagombea wwu
binafsi walio na uwezo kutumikia nchi wanaogombea uongozi wa kisiasa miongoni
wa makundi ya watu wenye ulemavu ili kuingia katika vikao vya maamuzi ambavyo
ni Bunge, Halmashauri/Manispaa, Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji.
2. Kila
panapotokea Rais, Waziri au mkuu yoyote wa kisiasa, Mtunga sera, na mtoa
maamuzi anakuwa na fursa ya kuteua
mtanzania kufanya kazi za umma, atawasiliana na Mamlaka mahsusi iliyowekwa ili kuona uwezekano wa kuteua pia mtu mwenye
ulemavu.
3. Watu wenye ulemavu watafaidika na
rasilimali za nchi kutoka Serikalini
katika ngazi zote (Serikali kuu na Halmashauri/Jiji/Manipaaa) itatoa ruzuku
asilimia 10% ya mapato kwa vyama vya watu wenye ulemavu ili viweze kuendesha
shughuli zao kimaendeleo na kupunguza
utegemezi katika jamii. Vigezo kuzingatiwa chini ya mamlaka husika.
4. Huduma zote za umma itakuwa ni bure
kwa watu wenye ulemavu, serikali itawajibika kugharamia huduma zote kwa
asilimia 100%.
5.
Kupitia
mamlaka husika, Serikali itawezesha tafiti kwa wingi na za kutosha zinazohusu watu
wenye ulemavu ili waweze kupanga maendeleo yao kwa uhakika, kuwa na taarifa za madai ya kueleweka,
wasionekane kama watu wa kulalamika
tu na wasio na hoja za msingi. Hii ni sehemu mojawapo ya wajibu.
Tafakari!!
1.
Hakuna chochote kuhusu sisi bila sisi
kushirikishwa!!!!!!
2.
‘’Tusisubiri maamuzi yafanywe wengine
kwa niaba yetu kisha tunaanza kulalamika kuhusiana na maamuzi hayo’’ ( Mwl JK.
Nyerere)
|
Read More ->>