Tuesday, September 17, 2013

TUMEKUELEWA SANA RAPPER STAMINA KWA UJIO WA "KABWELA FOUNDATION"




Usije kushangaa pale ambapo utamuona Rapper Stamina mtaani kwako akifanya shughuli za kijamii, kwasababu hivi sasa ameamua kuanzisha taasisi yake binafsi (NGO) aliyoipa jina la Kabwela Foundation.



"Ni Foundation ambayo nimeianzisha yaani ni kampuni kabisa ambayo tayari nimeshaisajili, na itakuwa inajihusisha zaidi na maswala ya kijamii, hasahasa kuwatembelea walemavu, maana kumekuwa na taaisisi nyingi ambazo zimekuwa zikiwaangalia sana watoto yatima, sasa mimi nitakuwa nikiwaangalia zaidi walemavu, sio yatima, kuna walemavu wana wazazi wao lakini hawajiwezi" alisema Stamina.
Aliongeza kwa kusema mpaka sasa tayari ameshapata atakaokuwa akishirikiana nao ambao ni wasanii wenzake, Young killer, G Warawara, Joe makini pamoja na Godzilla, ambapo atakuwa akitembelea kituo kimoja katika mkoa mmoja kila mwisho wa mwezi, na baada ya miezi 12 atakuwa ametembelea mikoa 12.

Umeeleweka sana!!! Jamii ya watu wenye ulemavu inakupongeza na kukuunga mkono katika juhudi zako.

Kindly Bookmark this Post using your favorite Bookmarking service:
Technorati Digg This Stumble Stumble Facebook Twitter
YOUR ADSENSE CODE GOES HERE

0 comments:

Post a Comment

 

| DISABILITY IN TANZANIA INFORMATION PLATFORM © 2012. All Rights Reserved |Designed by MIRAMBO GROUP | Back To Top |