Naitwa Christina Mauma mkazi wa kijiji cha
Kiara, nina ulemavu wa macho na sifanyi kazi.
Nina mtoto mmoja ambaye naishinaye
na kumtunza. Ulamavu nilionao nilizaliwanao.
Katika maisha ya kila siku nakumbana na
changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukosa msaada wa kumpeleka mtoto
shule. Miundombinu kutokua rafiki na ukosefu wa huduma tengamavu kwa watu wenye
ulemavu.
Naishauri jamii kuwapenda na kuwathamini watu
wenye ulemavu. Watu wenye ulemavu ni sawa na watu wengine wanahitilafu ndogo tu
katika viungo vyao ila wanahitaji kupendwa na kuthaminiwa kama watu wengine.
Serikali ijitahidi sana kuwajali na
kutekeleza mahitaji ya watu wenye ulemavu kwa vitendo isiishie kuzungumza
kwenye majukwaa tu.
Walemavu wenzangu wajitahidi kua karibu na
jamii na tusijiweke mbali na hata katika kazi tusaidiane kwa pamoja ili
tusiendelee kuonekana kua tuko nyuma sana.
Mashirika na asasi mbalimbali wajitahidi
kuzidi kuwatia moyo watu wenye ulemavu bila ubaguzi. Pia mashirika yanapokua
yanaita wawakilishi wa kuwasaidia katika shughuli mbalimbali wilayani na
mikoani wajitahidi kuwahusisha hata walemavu wasio wafanyakazi. Kitendo cha
kuwatumia wafanyakazi pekee kwa mfano; walimu ni kuwanyima walemavu wasio na
ajira fursa ya kujifunza na kutetea haki zao.
0 comments:
Post a Comment