Naitwa Donatus Masau ni mwenyekiti wa CHAWATA
wilaya ya Musoma vijijini, nimeoa na ninawatoto saba (7).
Kwaufupi nilizaliwa
nikiwa mzima lakini katika udogo wangu nilianza kuugua homa, baada ya kupelekwa
hospitali nikagundulika kua na ugonjwa wa Polio ambao ulipelekea miguu yangu
yote miwili kushindwa kufanya kazi. Baada ya kupelekwa kwa waganga wa kienyeji
ndo nikabahatika kupona mguu mmoja.
Katika mchakato wakuliendea swala la ndoa
nilipata ushirikiano mzuri kutoka kwa wazazi na familia yangu. Baada ya
kumaliza shule nilishauriwa kuoa, bahati nzuri akapatikana mchumba akaposwa,
mahali yakatolewa na tukaoana mwaka 1987na nilifunga ndoa ya kikristu.
Kwakweli mtu mwenye ulemavu tukubali
tusikubali inafikia hatua mpaka jamii ije kukuheshimu na kukuthamini ni pale
unapokua unajijari we mwenyewe. Heshima yangu ya kwanza nimejikita sana kwenye
ushauri, mwenzangu akikosea najaribu kumweleza kwamba hiki ulichokifanya sio
sawa. Hali hii ilienda mpaka jamii yangu wakaona kuna haja ya kuniteua na
kunipa ukatibu wa ukoo na hivyo naratibu shughuli zote za ukoo wangu.Kwa hali
hiyo naona kama naenda vizuri na jamii yangu na wanakuja kuniomba ushauri wa
mambo mbalimbali na tunaheshimiana kwakweli.
Kwa ujumla ndoto zangu ni kuona hakuna
unyanyasaji kwa wenzangu na ikitokea nawahi haraka kutoa ushauri. Kwa mfano
kama walemavu wenzangu najaribu sana kutafuta njia za kuwasaidia ili kutatua
matatizo yanayo wakabili ili tuwe kwenye mtazamo mzuri wa maisha. Ulemavu sio umaskini ila ni bahatimbaya kua kunabaadhi ya
viungo vinakua na hitilafu ila vichwa vinafanya kazi, tunaweza tukakaa tukabuni
na kufanya maendeleo kama watu wengine.
Naiomba jamii itambue kwamba
walemavu ni binaadamu kama walivo wao na wanataka heshima wathaminiwe, hivyo
ione umuhimu wa kuwapeleka shuleni ili wapate elimu hii itawafanya wafikie
hatua ya kua msaada katika jamii zao.
Taasisi za kiraia napenda kuzishauri kua
zitambue yakwamba idadi kubwa ya walemavu wako vijijini hivyo zione umuhimu wa
kufanya mahusiano mazuri na vijiji ambako walemavu wanahitaji misaada
mbalimbali. Waje vijijini kuwaelimisha na kuwapatia mwanga watu wenye ulemavu
kuliko kuishia mjini pekeake ambako unakuta idadi ya walemavu sio kubwa kama
vijijini.
Walemavu nawashauri kujenga tabia ya kupenda
sisi kwa sisi, mara nyingi sana mnapokua mnapendana ni rahisi kusaidiana kwenye
mambo mbalimbali. Mlemavu lazima asiwe na tabia ya kuwabagua watu wengine,
awapende na hii itapelekea watu kumsaidia. Lazima mlemavu aoneshe uwezo wa
kutenda na sio kufanya majungu. Kitu kinachotualibia sana nikwamba watu
wanasema sisi walemavu ni wakorofi! La! Ukorofi wetu unatokea pale ambapo
itikadi yangu na yakwako zitakapo tofautiana, kwahyo mlemavu kama mlemavu
shirikishwa na kubali mabadiliko.
Serikali naiomba iwajali sana walemavu, kwa
mfano serikali imeweka sheria ya kuwasaidia na kuwalinda walemavu lakini haikuweka angalizo la je wasipolindwa nini
kifanyike? Sasa ni sheria gani nitatekelezwa bila kanuni? Kwahyo naishauri
serikali iweke mpangilio mzuri wa kuwalinda na kuwasaidia walemavu sababu
hatuna sehemu yoyote ya kujikita kama sio huko serikalini.
0 comments:
Post a Comment