YOHANA
CHACHA
Naitwa Yohana Chacha ni mkazi wa wilaya ya
Butiama, kijiji cha Makutano. Mimi sina familia kutokana na halingumu ya
kiuchumi na mzaingira tunayoishi. Nina ulemavu wa macho na nilizaliwa nikiwa na
hali hiitangu tumboni mwa mama.
Kwakipindi kilichopita nilikua nafanya
biashara ndogondogo (kioski) ila kutokana na matatizo ya hapa na pale mtaji
wangu ukawa umeisha na sasahivi sina kazi kabisa.
Changamoto ninazo kumbana nazo ni kwa upande
wa jamii inayotuzunguka kutokutukubali kama binaadamu kamili. Nashindwa kuelewa
chanzo cha tatizo hili, sijui ni elimu ndogo ama nini?. Unajua kwa huku kwetu
vijijini swala la elimu kwa jamii nikama halipo, kwahiyo wanatuchukulia sisi
walemavu kama watu tulioumbwa kwa bahati mbaya au matunda ya laana.
Kutokua na fursa katika mambo
mbalimbali kinaweza kua ni kichocheo kingine cha kutufanya tusikubalike katika
jamii.
Jamii inatuchukulia kama mzigo, hata lile ambalo ungewezeshwa ukaweza linakua
ni vigumu kwa mlemavu kuwezeshwa. Namshukuru Mungu kuona mpaka leo bado nipo
pamoja na mambo mengimengi niliyo kumbananayo.
Kinachotakiwa kwa jamii, ingefaa kwanza
vyombo vya habari (radio, TV, pamoja an magazeti) waweze kutoa elimu kwa jamii
za watu walio vijijini juu ya namna na jinsi ya kuishi na kuwathamini watu
wenye ulemavu kama watu wengine. Wasitudharau, kutunyanyapaa, kutukejeli wala
kututenga. Wafute mitazamo hasi waliyonayo dhidi yetu sisi watu wenye ulemavu.
Nawashauri wenzangu wenye ulemavu yakwamba
tufanye ushirikiano na kutengeneza sauti ya pamoja, ili kuwaeleza jamii
inayotuzunguka kwamba nasisi tunahaki na tunastahili heshima zote. Pamoja nakwamba tuna ulemavu lakini tuifanye jamii
itambue kwamba hata sisi tunaweza tukatoa mawazo yakasikilizwa na tunaweza
tukafanya kitu kikaonekana. Tusiwe watu tegemezi kila wakati.
Naishauri serikali isaidie katika kuielimisha
jamii kuhusu maswala ya watu wenye ulemavu. Msisitizo mkubwa uwekwe kwa jamii
za wanaoishi vijijini na isiishie tu mijini kama ilivo sasa. Ukizunguka katika vijiji utakuta kuna walemavu ambao
hawapewi fursa yoyote, hata mgeni akifika nyumbani utakuta mlemavu anafichwa
ndani. Mimi kunakipindi hali hiyo ilinikuta lakini nilipambana
nayo. Serikali izunguke na kuwahamasisha wazazi wenye watoto walemavu
kuwapeleka watoto wao shule. Serikali isiishie kutoa mikopo ya biashara kwa
watu wazima peke yao, itambue pia kua kuna jamii ya watu wenye ulemavu ambayo
ili iondokane na hali ya kuitwa ombaomba. Wakiwezeshwa wakapewa mikopo yenye
masharti nafuu wanaweza kufanya kitu kinachoonekana napia wakachangia katika
kulipa kodi pia.
2 comments:
Uko sawa kabisa bwana YOHANA
its fine
Post a Comment