Naitwa Mwita Charles kutoka katika wilaya ya
Bunda, nina umri wa miaka 14. Nina wazazi wote wawili lakini baba anasubuliwa
na matatizo ya akili kwa sasa hivyo naishi na mama. Ninasoma shule ya msingi na
niko katika darasa la sita (6).
Nina ulemavu wa viungo, nilizaliwa pasipokua
na mikono yote miwili.
Katika kusoma kwangu naandika kwa kutumia miguu. Jamii
iliyo nizunguka inanichukulia kawaida, hawanitengi wala kuninyanyapaa, nacheza
na kushirikiana na watoto wenzangu kama mtu wa kawaida.
Mahusiano ya mama na baba sio mazuri
kwasababu wakikutana wanaanza kupigana, baba anamkaba shingo mama kwasababu ya
tatizo la akili alilonalo. Mama anafanya kazi ya vibarua, anahangaika sana ili
kupata pesa ya kunitunza na kunisomesha.Maendeleo yangu darasani ni mazuri sana
kwakweli. Natamani siku moja nije kua Rais wa nchi hii.
Naishauri serikali iwaongoze watu vizuri na
kuwasaidia maskini. Pia naiomba Serikali iwatunze, kuwasomesha na kuwasaidia
watu wenye ulemavu kama mimi.
0 comments:
Post a Comment