Amina
Mwamkinga alisema tangu tarehe tisa alipofukuzwa bwenini na wanafunzi wenzie
wakitaka aondoke shuleni hapo wakimtuhumu kuwa mchawi majira ya usiku hali
iliyomlazimu kuomba hifadhi kwa mlinzi aliyemkubalia na kukesha naye hadi
asubuhi hali iliyopelekea kupigwa na baridi kali kutokana na kukosa nguo
za kujisitiri kama Shuka nk.
Hapa Amina
akimsimulia mkasa mzima mwandishi wa Mbeya yetu Joseph Mwaisango mara baada ya
kupata maelezo yote ya Amina mwandishi alimpigia simu katibu wa chama cha
maalbino mkoa wa Mbeya afike ofisi ya Mbeya yetu ili wasaidiane kutatua tatizo
hilo.
katibu wa
Chama cha Albino Mkoa wa Mbeya, Wiliamu Simwale akiwa makini kumsikiliza
Amina katika ofisi ya Mbeya yetu
KATIKA Hali isiyokuwa ya Kawaida Uongozi wa Shule ya
Sekondari Hollwood iliyoko Mlowo Wilayani Mbozi Mkoa wa Mbeya imemsimamisha
shule Mwanafunzi wa kidato cha tatu kwa takribani Miezi Miwili kwa madai kuwa
anajihusisha na imani za Kishirikina.
Mwanafunzi huyo aliyejulikana kwa jina la Amina
Mwankinga(20) ambaye ni mlemavu wa ngozi(Albino) alisimamishwa shule na uongozi
wa Shule hiyo tangu Machi 9, Mwaka huu baada ya uongozi wa Shule hiyo kupata
taarifa kutoka kwa Wanafunzi wakimtuhumu Mwenzao huyo kuwa ni Mshirikina.
Uongozi wa Shule hiyo baada ya kupata taarifa hizo
ulimwamuru mhanga wa tukio hilo kuondoka Shuleni hapo pasipo kufuatilia na
kujua ukweli wa jambo hilo na kupata udhibiti hivyo kumwacha Mwanafunzi huyo
akizurura mitaani asijue hatma ya maisha yake.
Mhanga wa tukio hilo Amina Mwankinga alisema tangu tarehe
tisa alipofukuzwa bwenini na wanafunzi wenzie wakitaka aondoke shuleni hapo
majira ya usiku hali iliyomlazimu kuomba hifadhi kwa mlinzi aliyemkubalia na
kukesha naye hadi asubuhi hali iliyopelekea kupigwa na baridi kali
kutokana na kukosa nguo za kujisitiri kama Shuka nk.
Anasema kutokana na hali hiyo Walimu pamoja na uongozi wa
Shule hiyo haukuchukua hatua yoyote jambo lililomlazimu kuondoka Shuleni
hapo baada ya kukosa msaada ambapo alirejea Jijini Mbeya anakoishi na
Binamu yake.
Binti huyo anayesomeshwa na Shirika la Under the
SameSun iliyoko Jijini Dar Es Salaam aliwaambia waandishi wa habari
kuhusu mkasa uliompata huku akiomba msaada kwa wasamaria wema kumtafutia Shule
ili aendelee na masomo kwa ajili ya kujiandaa na mtihani wa kidato cha nne
Mwakani.
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya HollyWood Ambukeghe Mtafya,
alipopigiwa simu kuhusu tuhumahizo alikiri kulijua suala hilo na kwamba
walimrudisha mwanafunzi huyo nyumbani ili kumnusuru na kipigo kutoka kwa
wanafunzi wenzie na kuongeza kuwa aliambiwa atafute shule nyingine ili ahamie.
Naye
katibu wa Chama cha Albino Mkoa wa Mbeya, Wiliamu Simwale alisema
alikuwa halijui suala hilo na kwamba kama lingekuwa suala liko nyeti
angejulishwa yeye juu ya hatua zilizofikiwa ambapo Uongozi wa Shule umeendelea
kupokea fedha za malipo ya Mwanafunzi pasipo kutoa taarifa kwenye shirika
linalolipa.
Mlezi wa Wanafunzi hao kutoka Shirika la Under the Samesun
Omary Mfaume amesema kwamba hana taarifa zozote kuhusiana na tukio hilo
na kuongeza kuwa anawasiliana na uongozi wa Shule moja kwa moja ili umweleze
juu ya kilichotokea ili taratibu za kumtafutia Shule nyingine zifanyika haraka
ili Mwanafunzi aendelee na masomo kama kawaida.
Na Mbeya yetu.
0 comments:
Post a Comment