Usije kushangaa pale
ambapo utamuona Rapper Stamina mtaani kwako akifanya shughuli za kijamii,
kwasababu hivi sasa ameamua kuanzisha taasisi yake binafsi (NGO) aliyoipa jina
la Kabwela Foundation.
"Ni Foundation
ambayo nimeianzisha yaani ni kampuni kabisa ambayo tayari nimeshaisajili, na
itakuwa inajihusisha zaidi na maswala ya kijamii, hasahasa kuwatembelea
walemavu, maana kumekuwa na taaisisi nyingi ambazo zimekuwa zikiwaangalia sana
watoto yatima, sasa mimi nitakuwa nikiwaangalia zaidi walemavu, sio yatima,
kuna walemavu wana wazazi wao lakini hawajiwezi" alisema Stamina.
Aliongeza kwa kusema
mpaka sasa tayari ameshapata atakaokuwa akishirikiana nao ambao ni wasanii
wenzake, Young
killer,
G Warawara, Joe makini
pamoja na Godzilla, ambapo atakuwa akitembelea kituo kimoja katika mkoa mmoja kila
mwisho wa mwezi, na baada ya miezi 12 atakuwa ametembelea mikoa 12.
Umeeleweka sana!!! Jamii
ya watu wenye ulemavu inakupongeza na kukuunga mkono katika juhudi zako.
0 comments:
Post a Comment